Polisi 130 wa Afghanistan wajisalimisha kwa magaidi wa Taleban
Kwa akali polisi 130 wa serikali ya
Afghanistan wamejisalimisha kwa wanachama wa kundi la kigaidi na
Kiwahabi la Taleban kufuatia kudhibitiwa mji wa Kohestan mkoa wa Faryab,
kaskazini mwa Afghanistan.
Abdul-Karim Yuresh, msemaji wa
polisi wa mkoa wa Faryab sambamba na kuthibitisha habari hiyo amesema
kuwa, polisi wengine 200 bado wanazingirwa na wapiganaji wa kundi hilo
la Kiwahabi katika eneo la Ghaleh Kheyr Abad la mji wa Kohestan. Taarifa
iliyotolewa na kundi la Taleban imesema kuwa, linaendeleza mwenendo
wake wa kuwafanya askari wote wa nchi hiyo wajisalimishe kwake.
Siku mbili zilizopita, kundi la hilo
lilishambulia miji ya Bilchiragh na Dolatabad katika mkoa wa Faryab,
kaskazini mwa nchi hiyo ambapo katika hujuma hiyo lilidhibiti vijiji na
vituo saba vya polisi. Kadhalika kundi hilo lilishadidisha mashambulizi
ndani ya wiki iliyopita kuvilenga vituo vya polisi vya wilaya ya Qaysar
katika mkoa wa Faryab na kuua polisi kadhaa. Hii ni katika hali ambayo
hadi sasa vyombo vya habari vimeripoti kuendelea mapigano makali kati ya
askari wa serikali na wapiganaji wa kundi hilo. Makundi ya kigaidi
yenye kufuata idolojia ya Uwahabi, hususan Taleban, al-Qaidah na Daesh
yanaendesha harakati zao nchini Afghanistan, licha ya uepo wa vikosi vya
jeshi kutoka nchi za Magharibi zikiongozwa na Marekani.
Marekani na washirika wake
waliishambulia Afghanistan mwaka 2001 kwa madai ya kukabiliana na
ugaidi, katika hali ambayo uepo wa askari hao wa kigeni nchini humo,
ndio umechangia ongezeko la ugaidi huo.
JIUNGE NASI AKISI TV KILA SIKU KUPATA HABARI ZA UHAKIKA Nini maoni yako? Weka comment yako hapa,
No comments