HATIMAYE T.I KAJIBU TUHUMA ALIZOPEWA NA ROB KARDASHIAN
Wiki iliyopita kwenye mtandao wa instagram kulitokea utata kati ya Rob Kardashian na aliyekuwa mpenzi wake Blac chyna na kupelekea Rob Kardashian kutuma picha za utupu za Blac Chyna mtandaoni hali iliyo ilazimu wamiliki wa mtandao wa Instagram kuifungia akaunti ya Instagram ya Rob.
Wakati Rob Kardashian anatuma picha za utupu za Blac Chyna rapa T I aliingilia kwa kumuuliza Rob Kardashian kuwa ni kwa nini habari za kifamilia anazileta kwenye mitandao ya kijamii hali iliyomfanya Rob Kardashian kumjibu T I kwa kumwambia kuwa asijifanye msafi wakati aliwahi kufanya mapenzi na Blac Chyna na mkewe Tiny kwa pamoja.
Akihojiwa na kituo cha TMz T.I aliulizwa kuhusu tukio hilo na T .I alijibu kwa kusema" Rob is gonna have hard time with women.he humiliated all of them and no woman will trust him" akiwa anamaanisha Rob atapata shida sana kuwa na wasichana maana alichofanya amewadhalilisha wanawake wote hakuna mwanamke atakae muamini tena huku akikanusha tuhuma za kufanya mapenzi wakiwa watatu na Mkewe na Blac Chyna.

No comments