SAFARI NI HATUA
Asubuhi
kumekucha, Majogoo yanawika,
Muda wa Mungu kumcha, Sisi tulosalimika,
Tunashukuru kukucha, Tele ikiwa mizuka,
Ewe
Msafiri leo, nenda urudi salama
Kengere
ya kanisani, yatua kutuamsha
Kuwaita
waumini, usingizi ukakwisha
Nina
simu mkononi, na kisha nikaiwasha
Ewe
Msafiri leo, nenda urudi salama
Moyo
umenisituka, kukutana na ujumbe
Jasho
lanitiririka, laweza jaza vikombe
Mpenzi
liye sirika, kanitumia ujumbe
Ewe
Msafiri leo, nenda urudi salama
Muheza naelekea, Mapema nilikwambia,
Shughuli kusherekea,
rafiki unamjua,
Siku
nitaporejea,kuna jambo takwambia
Kwaheri
wangu lazizi, nitarejea salama
Ndivyo
ilivyosomeka, meseji yake ya mwisho.
Hili si lakupingika, nikahisi
ni michosho,
Moyo ulinidundika, kwanini ajitie ficho,
Moyo ulinidundika, kwanini ajitie ficho,
Ewe
Msafiri leo, nenda urudi salama
Safari ndefu hatua, nenda ufike salama
Sawa
nimeshatambua, ufikapo utasema
Nami
nipate kujua, ujumbe nikautuma
Ewe
Msafiri leo, nenda urudi salama
Nikaamka
vizuri, kwa kudra za Maulana
Kazi
nikazikabiri, ni jambo langu la mana
Siku
iende vizuri, mwana wa Juma Kibwana
Ewe
Msafiri leo, nenda urudi salama
Yakakatika
masaa, ujumbe nikautuma
Sebuleni
nimekaa, tivii ninatazama
Nakujulia
wasaa, kama umefika vema
Ewe
Msafiri leo, nenda urudi salama
Mpenzi
wangu ufizi, mie meno sina hali
We
mganga mfawizi, nijibu vipiyo hali
Ewe
Msafiri leo, nenda urudi salama
Ghafla
ninasitushwa, taarifa ya habari
Puu
nikaangushwa, nishapatwa na hatari
Nguvu
zimepunguwa,nashindwa kujisitiri
Ewe
Msafiri leo, nenda urudi salama
NB:
Simulizi kwa njia ya mashairi, haya ni masimulizi ya kusisimua ya visa vya
kweli na vya kubuni, vitakuwa vinakujia hapahapa AKISITV.COM kwenye kurasa ya
UTAMU WA FASIHI,
Anza
sasa kufatilia kila siku ili uweze kuonja na kuufaidi utamu wa Fasihi
No comments