-->

Header Ads

MAHUSIANO YA RIHANNA NA CHANCE THE RAPPER MITANDAONI

Mwanadada wa miondoko ya R&B Rihanna na rapa Chance the rapper wametajwa na Jarida la Time kua ndio mastaa wanao ongoza kuwa na ushawishi mkubwa mitandaoni.

Jarida hilo la Time lilitoa orodha ya watu 25 wenye ushawishi mitandaoni ikiongozwa na Rihanna na Chance the rapper. 

Jarida hilo limesema kuwa mwanadada Rihanna anaushawishi pia kwenye masuala ya mavazi kwani watu wengi hupendelea kuvaa kama jinsi Rihanna anavyovaa na kupost picha kwenye mitandao ya kijamii  kama Facebook na Instagram.

Pia jarida hilo limesema hata habari ambazo zinatolewa na mastaa hao zimekua na ushawishi mkubwa kwa watu mitandaoni.

Mastaa wengine waliotajwa ni pamoja na Harry potter,Katty Perry na Michelle Obama pamoja na wengine.

No comments

Powered by Blogger.