-->

Header Ads

RASMI; NGOMA ASAINI YANGA.. WATAMBA USAJILI BADO UNAENDELEA

Baada ya tetesi za muda mrefu na kusumbua katika vichwa vya habari hatimaye Donard Ngoma asaini miaka miwili jangwani.

Ngoma amesaini mkata huo mchana huu ambao utamuweka jangwani kwa miaka miwili zaidi. huku akifuata nyayo za Hamis Tambwe ambaye pia kasaini miaka miwili ya kukitumikia kikosi hicho.

Mwanzoni vyombo vya habari viliingizwa chaka na mtandao wa kickoff was south Afrika ambao ulilipoti kuwa Ngoma amesaini katika klabu ya Polokwame City.

Hivyo taarifa rasmi ni kuwa Ngoma sasa ni mchezaji halali wa Tanga na kuvunja tetesi za kuhamia kwa watani wao Simba.

Vilevile Yanga wametamba kuwa bado usajili unaendelea na siku ambayo watatangaza wachezaji wao waliosajiliwa nchi itasimama.

No comments

Powered by Blogger.