CHILE YATINGA FAINALI KOMBE LA MABARA MARA BAADA YA KUICHAPA URENO 3-0 KUPITIA MIKWAJU YA PENALT.

Chile yafanikiwa kutinga fainali ya michuano ya kombe la mabara baada ya kuiondosha Ureno kwa penalti 3-0.
Katika mechi hiyo iliyochezwa jana mlinda mlango wa Manchester City Claudio Bravo alikua shujaa wakati timu yake ya Chile ilipoiondosha Ureno katika hatua ya nusu fainali na kutinga fainali.


Bravo aliokoa mikwaju ya penalti iliyopigwa na Ricardo Quaresma, Joao Moutinho na Nani huku Chile wakifanikiwa kupata penalti tatu zilizoipa njia ya moja kwa moja chile kuingia hatua ya fainali. Ikumbukwe pia sio mara ya kwanza kwa Bravo kupangua mikwaju ya penalt pia alishawahi kuokoa mikwaju ya penalti akiwa na timu yake Manchester city mnamo Oktoba mwaka jana dhidi ya Tottenham. Kutokana na matokeo hayo sasa Chile itakutana na Ujerumani ama Mexico katika fainali siku ya Jumapili katika mji wa St Petersburg.

No comments