SERENGETI BOYS YAUA GABON, ANGOLA WAPAGAWA
Timu ya Taifa ya vijana chini ya umri wa miaka 17 Serengeti boys leo wamekitupa dimbani dhidi ya Angola, Serengeti Boys ambao wamemenyana na Angola kunako dimba la L'Amitie mjini Libreville katika mchezo wake wa pili wa Kundi B Fainali za Vijana Afrika chini ya umri wa miaka 17 zinazeondelea .
Serengeti boys wamekingia kifua vijana wa Angola kwa mabao 2-1, Serengeti Boys ndio waliokuwa wa kwanza kutikisa nyavu za Angola kunako dakika ya 5 ya kipindi cha kwanza bao ambalo lilifungwa na mchezaji Kelvin Nashon Naftali.
mchezo uliendelea kwa kasi lakini kunako dakika ya 17 kipindi cha kwanza vijana wa Angola walijibu mashambulizi na kutikisa nyavu za serengeti Boys.
mpira ulienda mapumziko huku timu zote mbili zikiwa sare ya mabao 1-1,
baada ya mapumziko timu mchezo ulirudi kwa kasi huku timu zote mbili zikiwa na uchu wa kutafuta bao la pili, lakini kunako dakika ya 68 kipindi cha pili Abdul Hamisi alitikisa nyavu za Angola na kuipatia serengeti Boys Bao la pili.
hivyo kutokana na matokeo hayo Serengeti Boys inapata alama nne (4) baada ya mchezo wao wa kwanza dhidi ya Mali ambapo walitoa sare ya bila kufungana.
Hivyo serengeti Boys wamebakisha Mchezo mmja ambao watamenyana na Niger.
Boys wako katika Kundi B na timu za Mali, Angola na Niger.
KIKOSI CHA SERENGETI BOYS KILICHOCHEZA
1. Ramadhan Awm Kabwili
2. Kibwana Ally Shomary
3. Nickson Clement Kibabage
4. Dickson Nickson Job
5. Ally Hussen Msengi
6. Enrick Vitalis Nkosi
7. Abdul Hamis suleiman
8. Ally Hamis Ng'anzi
9. Yohana Oscar Mkomola
10. Kelvin Nashon Naftali
11. Assad Juma Ally
KIKOSI CHA AKIBA
1. Samwel Edward Brazio
2. Kelvin Deo Kayengo
3. Israel Patrick Mwenda
4. Syrprian Benedicto Mtesigwa
5. Marco Gerald Mhilu
6. Shabaan Zubery Ada
7. Abdalah Mohamed Rashid
8. -Bakari Said Mussa
9. Muhsin Malima Makame
10. brahim Abdallah Ali
No comments