YOUTUBE YAMSUJUDU CHRIS BROWN KWA 'DIAMOND' NA BARUA
Mtandao wa YouTube leo umeamua kumtunuku msanii wa marekani miondoko ya rnb kwa kumuandikia BARUA na kumzawadia zawadi ya Almasi {diamond} nzuri ya bei mbaya..
Youtube waliamua kumpa heshima kubwa chris brown kutokana na ukweli kuwa chris ndiye mtu anayeongoza kuwa na subscribers wengi zaidi duniani na anatajwa kuwa msanii anayeongoza kwa kupiga mkwanja mwingi zaid kupitia youtube.
Chris Brown kupitia mtandao wake wa instagram ameweka barua hiyo na wazi na kuonesha furaha yake kwa heshima aliopokea kutoka YouTube kwa kusema 'thank you YouTube '.
Mashabiki wengi wa Chris Brown pia wamekuwa na furaha kufuatia icon huyo kupata heshima hiyo kubwa..
Nimekuwekea barua ya youtube kwa chris brown ambayo ilipostiwa kupitia ukurasa wa instagram wa Chris, soma uone mwenyewe.
Pia zawadi ya diamond ya thamani kubwa hii hapa.
No comments