Mvua yaleta maafa mengine, yaua wawili, yajeruhi wanane
Watu wawili wamefariki dunia baada ya kusombwa na maji huku wanane wakijeruhiwa kwa kuangukiwa na kuta kufuatia mvua zinazoendelea kunyesha.
Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Tanga, Benedict Wakulyamba alisema jana kuwa watu wawili walifariki asubuhi katika Kijiji cha Magila, Kata ya Mkumbara wilayani Korogwe..
Aliwataja waliofariki kuwa ni Happiness Mvita (24) na mwanaye Prisca Lugi (4).
Wakulyamba alisema miongoni kwa waliojeruhiwa yupo mtoto mwenye umri wa chini ya mwaka mmoja na kwamba majina ya majeruhi wote yatatolewa baadaye.
“Majeruhi wamelazwa katika Hospitali Wilaya ya Korogwe ya Magunga kwa ajili ya matibabu,” alisema Kamanda Wakulyamba na kuwataka wananchi kuwa waangalifu kipindi hiki cha mvua.
Mbunge wa Korogwe Vijijini, Stephen Ngonyani alitoa pole kwa familia za marehemu.
source : Mwananchi
JIUNGE NASI AKISI TV KILA SIKU KUPATA HABARI ZA UHAKIKA Nini maoni yako? Weka comment yako hapa,
No comments