-->

Header Ads

CHINA YAUNGANA NA MAREKANI KUIADHIBU KOREA KASKAZINI

Mdau wa AKISITV bila shaka umekua ukifuatilia kile kinachoendelea kati ya Marekani na Korea ya Kaskazini.

Kumekuwepo na vitisho vya hapa na pale kutoka kwa Marekani kwa Korea ya Kaskazini kuacha mara moja majaribio yake ya silaha za nyuklia.

Hatahivyo Korea ya Kaskazini chini ya Raisi wake Kim Jong Un imepinga agizo hilo na kusema kuwa itaendelea kufanya majaribio yake kila wiki.

China imekua moja ya taifa lililounga mkono marekani katika kupambana na mpango wa nyuklia wa Korea Kaskazini.

Rais wa Marekani, Donald Trump amemsifu rais wa China, Xi jinping kwa kuunga mkono jitihada hizo.

Trump amesema kupata ushirikiano huo wa kupambana na Pyongyang ilikuwa muhimu kuliko kuishinikiza Beijing kuhusu masuala ya biashara.

Rais Donald Trump amesema aliamini kuwa Rais Xi alikuwa akiishinikiza Korea kaskazini, ikitaka, mazungumzo yafanyike kuhusu silaha za Nuklia za Kim Jong Un.

Trump ametahadharisha kuwa mgogoro wowote wa kijeshi na Korea kaskazini unaweza kugharimu maisha ya mamilioni ya watu.

Trump aliyasema hayo kwenye mahojiano na chombo cha habari cha CBS cha Marekani ambapo alizungumzia hali ya mvutano iliopo kati ya nchi yake na Korea kaskazini.

No comments

Powered by Blogger.