-->

Header Ads

Watu 10 wameuawa kwenye vituo viwili vya treni URUSI



Takriban watu 10 wameuawa kufuatia milipuko iliyotokea kwenye vituo viwili vya treni ya chini ya ardhi mjini St Petersburg nchini Urusi.

Mashirika ya habari yanaripoti kuwa milipuko hiyo ilitokea kituo vya Sennaya Ploschad na kingine kilicho karibu cha Tekhnologichesky Institut, kati kati mwa mji.

Picha zilizowekwa kwenye mitandao ya kijamii zilionyesha behewa kati kituo cha Sennaya likiwa limebaribiwa na watu waliouawa wakiwa karibu.

Rais wa Urusi Vladimir Putin anasema uchunguzi unafanywa.


Vituo vya habari vya Interfax na RIA viliripoti kuwa takriban watu 50 walijeruhiwa.

Mfumo wote wa usafiri wa treni ya chini ya ardhi mjini humo kwa sasa umefungwa na maasfisa wa usafiri wanasema kuwa wameongeza huduma za usalama.

Mwaka 2009 mlipuko ulitokea kwenye treni moja ya mwendo wa kasi kati ya miji ya Moscow na St Petersburg, ambapo 27 waliuawa na wengine 130 kujeruhiwa.

BBC

No comments

Powered by Blogger.