NEEMA YATUA JANGWANI, WAKENYA KUMWAGA BILIONI YANGA
*WAKENYA HAO JANGWANI*
Timu ya Yanga SC ambayo kwa sasa haipo vizuri kifedha baada ya mwenyekiti wao ambaye ndiye mfadhili, Yusuf Manji kupata matatizo na kutokuwa karibu na timu mpaka kupelekea baadhi ya wachezaji kugoma kutokana na kucheleweshewa mishahara yao, huenda wakaondokana na hali hiyo baada ya kutokea kwa mabosi wanaotaka kuidhamini klabu hiyo.
Kampuni ya SportsPesa kutoka Kenya wanatarajia kuingia mkataba wa miaka mitano na Yanga wenye thamani ya Billion 4.5 ambao kwa mwaka utakuwa na thamani ya TSh. milioni 900.
No comments