-->

Header Ads

MILIONI 300 ZA TFF ZAWAOKOA WACHEZAJI HAWA WA YANGA

Wachezaji 11 wa Yanga ambao wamechelewa Ndege huko Algeria walikokwenda kucheza mechi ya kimataifa ya Kombe Shirikisho barani Afrika dhidi ya MC Alger na kutolewa kwa jumla ya mabao 4-1, sasa watarudi nchini Alhamisi ijayo baada ya shirikisho la soka Tanzania kuwalipia gharama za nauli za kurudi nchini baada ya kuchelewa ndege ambayo walipangiwa kupanda awali.

Msemaji wa TFF, Alfred Lucas amethibisha taarifa hiyo kwa kusema imewapasa kuwasaidia wachezaji wa Yanga waliokwama uwanja wa ndege kwa kuwa walienda kuwakilisha nchi hivyo shirikisho hilo limeona busara kuwachangia Yanga gharama za nauli za kurudia nchini.

Wachezaji walioachwa ni Donald Ngoma, Thaban kamusoko, Andrew Vicent ‘Dante’, Kevin Yondani, Haruna Niyonzima, Haji Mwinyi, Deogratius Munishi ‘Dida’, Deus Kaseke, Emanuel Martin na Juma Abdul.

Habari kutoka Algeria zinasema kwamba wachezaji hao sasa washakamilisha taratibu zote na watarejea nchini Alhamisi ambapo mechi yao ya Kombe la FA dhidi ya Prisons itachezwa Jumamosi yaani siku mbili baada ya kuwasili.

No comments

Powered by Blogger.