PROF. MAJI MAREFU AISHANGAA TAARIFA YA TAKUKURU
Korogwe.
Mbunge wa jimbo la Korogwe Vijijini Profesa Stephen Ngonyani(Profesa Maji marefu) amesema taarifa iliyotolewa na Taasisi ya kuzuia na kupambana na rushwa (Takukuru) mkoa wa Tanga wiki iliyopita kwamba Halmashauri za Wilaya,Miji na Jiji zinaongoza kwa rushwa haistahilikufumbiwa macho.
Alisema taarifa hiyo ilimshtua kwa sababu mafungu mengi yanayopitishwa na bunge hupelekwa Halmashauri kwa ajili ya kuendesha shughuli za maendeleo ya wananchi hivyo kama watumishi wake wanakosa uadilifu maana yake hata fedha hizo haziko katika mikono salama.
“Taarifa hiyo imenishtua kwa sababu inaonyesha baadhi ya watendaji katika halmashauri zilizopo mkoani kwetu hawaendi sambamba na Rais wetu John Magufuli ambaye hataki wananchi waombwe rushwa ili wapewe huduma”alisema Profesa Maji Marefu.
Alisema uchunguzi uliofanyika katika kipindi cha kuanzia Julai 2016 hadi Machi 2017 ni kwamba Takukuru ilimepokea jumla ya taarifa 222 za vitendo vya rushwa toka kwa wananchi wakilalamikia idara mbalimbali za Serikali.
Serikali za mitaa alisema inaongoza kwa kuwa na taarifa 99,huku idara za elimu zikiwa na malalamiko 28ikifuatiwa naafya yenye malalamiko 21,jeshi la polisi 14,idara za ardhi 11 na mahakama 11.
CHANZO: MWANANCHI
No comments