-->

Header Ads

KAGERA YAENDELEA KUISHIKA PABAYA SIMBA.

Katika sakata linaloendelea ambapo timu ya Kagera sugar imekata rufaa kupinga ushindi wa mezani uliopewa timu ya Simba. Simba walipeleka malalamiko yao kwa kamati ya masaa 72 wakidai kuwa timu ya Kagera sugar walichezesha mchezaji mwenye kadi tatu katika mechi iliyowakuatanisha vigogo hao ambapo ni kinyume na kanuni na sheria. Na kamati ilifikia maamuzi ya kuwapa ushindi wa mezani Simba.

Ikiwa ni muendelezo wa sekeseke hilo, Leo timu ya Kagera imetuma wajumbe watatu ambao wataudhulia kikao cha kamati ya sheria na hadhi ya wachezaji kitakachofanyika siku ya jumanne na kufanya tathimini ya kesi hiyo ilivyoendeshwa ili kujilidhisha na maamuzi yaliyotolewa na kamati ya masaa 72.

Hivyo inawaweka pabaya timu ya Simba ambayo imevuna pointi nne Katika mechi walizocheza kanda ya ziwa huku wakisubili maamuzi ya rufaa yao ambayo itawaweka mazingira mazuri ya kuchukua ubingwa msimu huu.

No comments

Powered by Blogger.