-->

Header Ads

BAADA YA YANGA KUTOLEWA, TANZANIA NDIO BASI TENA.

ALGERS, Algeria

BAADA ya wawakilishi pekee wa Tanzania waliokuwa wamebaki katika michuano ya Kimataifa timu ya Yanga kuondoshwa kwenye kombe la Shirikisho Afrika na MC Alger kwa kichapo cha mabao 4-0, Tanzania inakuwa imefunga rasmi ukurasa wa michuano ya kimataifa kwa upande wa klabu.

Katika mchezo wa awali uliofanyika kwenye uwanja wa Taifa Dar es Salaam wikiendi iliyopita Yanga iliibuka na ushindi wa bao moja hivyo kipigo cha leo kilichoiacha Tanzania bila mwakilishi yoyote kimewafanya watoto hao wa Jangwani watolewa kwa jumla ya mabao 4-1.

Wenyeji walicheza mchezo wa kasi kwa kulisakama lango la Yanga muda mrefu ambapo mpaka wakienda mapumziko walikuwa mbele kwa mabao mawili.

Mshambuliaji Bougueche Hajj alifunga bao la tatu dakika ya 65 na kuwavunja moyo kabisa wachezaji wa Yanga waliokuwa kwenye jitihada za kurudisha mabao mawili ya awali yaliyofungwa na Aouedj na Derrardja.

Katika mchezo huo uliopigwa kwenye dimba la Julai 5, 1962 Yanga walishindwa kufurukuta mbele ya wenyeji ambao walikuwa bora zaidi karibu kila idara ukilinganisha na mchezo uliopita uliofanyika jijini Dar es Salaam.

Huku wengi wakiamini mchezo utamalizika kwa mabingwa hao wa Tanzania kufungwa mabao matatu Aoudj aliwapatia bao la nne dakika ya 91 kufuatia wachezaji wa Yanga kufanya uzembe langoni kwao.

No comments

Powered by Blogger.