-->

Header Ads

Jeshi la Magereza kujenga kiwanda cha sukari


Morogoro. Jeshi la Magereza nchini limeanza kuimarisha  kujenga upya kiwanda chake cha viatu cha Karanga kilichopo wilaya ya Moshi mkoani Kilimanjaro na kuanzisha kiwanda kipya cha sukari katika gereza la Mbigiri mkoani Morogoro.
Ili kufanikisha hilo tayari Shule ya Sekondari ya Bwawani inayomilikiwa na jeshi hilo iliyopo Chalinze,mkoani Pwani imeanzisha mtaala wa masomo ya sayansi ili kuandaa wa vijana wa kufanya kazi viwandani.
Akizungumza na waandishi wa habari kwa niaba ya Kamishna Jenerali wa MagerEZA, Kamishna wa Utawala na Fedha, Gaston Sanga amesema mikakati hiyo inalenga kuunga mkono jitihada zinazofanywa na Serikali kutilia mkazo ukuaji wa uchumi kupitia viwanda.

source; mwananchi



JIUNGE NASI AKISI TV KILA SIKU KUPATA HABARI ZA UHAKIKA Nini maoni yako? Weka comment yako hapa,
Powered by Blogger.