Winnie Mandela alazwa hospitalini Johannesburg.
Shujaa aliyepinga ubaguzi wa rangi nchini Afrika Kusini Winnie Madikizela-Mandela, amelazwa hospitalii kwa kile kinachotajwa kuwa kufanyiwa uchunguzi wa kiafya.
Familia yake inasema kuwa alipelekwa hospitali ya Milpark mjini Johannesburg.
Mwezi Disemba mwaka uliopita, Bi Madikizela-Mandela alilazwa hospitali hiyo lakini kile kilichosababisha alazwe hakikutajwa.
Msemaji wake Victor Dlamini, aliambia BBC kuwa alikuwa ameenda kufanyiwa uchunguzi wa kawaida lakini madaktari wakaamua kumlaza.
Bi Madikizela-Mandela alikuwa mke wa Nelson Mandela, na alikuwa mwanamke wa kwanza mweusi kusajiliwa kama mhudumu wa kijamii nchini Afrika Kusini.
No comments