Libya: Uturuki ndio inayounga mkono makundi ya kigaidi yanayofanya jinai Libya
Msemaji wa wapiganaji wa serikali yenye makao yake huko mashariki mwa Libya ameiarifisha rasmi Uturuki kuwa ndio muungaji mkono mkubwa wa makundi ya kigaidi nchini humo.
Ahmed al-Mismari, amesema kuwa serikali ya Uturuki imekuwa ikiyaunga mkono kwa njia ya moja kwa moja makundi ya kigaidi nchini Libya kiasi kwamba, vibaraka wa Ankara na wengine kutoka Nigeria wamekuwa wakishirikiana na magaidi hatari wa Daesh kwa ajili ya kuchafua usalama wa Libya.
Baadhi ya wanamgambo wanaochafua usalama Libya
Al-Mismari ameongeza kuwa, licha ya uungaji mkono mkubwa wa baadhi ya nchi ikiwemo Uturuki kwa makundi ya kigaidi hususan Daesh huko Libya, lakini vita dhidi ya magaidi vinaelekea mwisho.
Msemaji wa wapiganaji wa serikali yenye makao yake huko mashariki mwa Libya, amesisitiza udharura wa kujisalimisha makundi ya kigaidi yaliyopo Tripol na kwamba silaha zao zinahesabika kuwa mali ya jeshi.
Jeshi la Libya
Ameongeza kuwa, utumiaji wowote wa silaha unahesabiwa kuwa wa kiadui na unaotakiwa kukabiliwa na jeshi la Libya.
Ni vyema kuashiria kuwa, Libya ina serikali mbili hasimu, moja ikiwa na makao yake mjini Tobruk na nyingine ya Umoja wa Kitaifa inayoungwa mkono na Umoja wa Mataifa.
No comments