-->

Header Ads

Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu: Uhuru wa kujieleza uko mashakani nchini Tanzania


Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu nchini Tanzania (LHRC) kimetangaza kuwa, haki ya uhuru wa kujieleza na kukusanyika iko shakani katika nchi hiyo ya Afrika Mashariki kutokana na kuwapo kwa udhaifu katika sheria mbalimbali.


Hayo yameelezwa na Ana Henga, Mkurugenzi wa Utetezi na Maboresho wa Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu nchini Tanzania (LHRC) wakati wakati wa uzinduzi wa Kampeni ya Kulinda Uhuru wa Kujieleza na Kukusanyika nchini humo.

Kampeni hiyo imeandaliwa na kituo hicho kupitia mradi wa uhakiki kwa kushirikiana na wadau washirika ambao ni Jukwaa la Wahariri Tanzania (TEF), Baraza la Habari (MCT), Policy Forum, Twaweza, Mtandao wa Jinsia Tanzania (TGNP), Kituo cha Demokrasia Tanzania (TCD), Shirika la Wanawake katika Sheria na Maendeleo Afrika (WiLDAF) na Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora na lengo lake ni kutoa elimu kuhusiana na haki ya uhuru wa kujieleza.


 Afisa huyo wa LHRC amesema kuwa, baada ya Serikali  ya Rais Magufuli kupiga marufuku mikutano ya kisiasa mpaka mwaka 2020, utaratibu wa kutoa taarifa kwa Jeshi la Polisi kabla ya kukusanyika sasa umegeuzwa na kuwa si taarifa tena, bali ni kuomba idhini au kibali jambo ambalo linapingana na katiba ya nchi.

Amesema kuwa, wameamua kuendesha kampeni hiyo baada ya kubaini changamoto kadhaa zinazofifisha uhuru wa kukusanyika nchini Tanzania ambazo ni uzuiaji holela wa mikusanyiko.

Kwa upande wake Theophil Makunga, Mwenyekiti wa Jukwaa la Wahariri Tanzania (TEF),  amesema kuwa, uhuru wa kujieleza na kukusanyika ni muhimu hasa kwa waandishi wa habari kwani huwarahisishia kupata habari.

source : radio tehran

No comments

Powered by Blogger.