KIGOMA : WANAFUNZI WAUGUA GHAFLA, WAZAZI WAWAKIMBIZA HOSPITALI
Wanafunzi wanaosoma katika Shule ya Msingi Munyika Kijiji cha Kajana tarafa ya Muyama wilayani Buhigwe mkoani kigoma wamekubwa na ugonjwa wa ajabu hali iliyowalazimu wazazi na walezi kufika shukeni hapo kwa ajili ya kuwapatia tiba mbadala na wengine 80 wapelekwa katika Zahanati ya Kijiji hicho baada ya kuzidiwa na maumivu ya kichwa, tumbo huku joto la miili yao ikiongezeka kila mara.
Akithibitisha hilo kwa njia ya simu, Mwalimu mkuu wa shule ya Msingi Mnyika Japheti Lukanka alikiri kutokea kwa tukio hilo, ambalo limejitokeza machi 6, mwaka huu, saa 1:30 asubuhi , hali iliyowalazimu baadhi ya wazazi kuwaombea ruhusa watoto wao wanaosoma katika shule hiyo ili kuwapatia matibabu.
Lukanka alisema kuwa wakiwa paredi katika zoezi la ukaguzi wa usafi , ghafla mwanafunzi mmoja alidondoka na kupewa huduma ya kwanza hatimaye alirudishwa nyumbani kwao kitendo kilichozidi kuwashtua ni pale wanafunzi wa darasa la sita walienda ofisini kwakwe na kuomba ruhusa kwa kuugua ugonjwa huo na kufika saa 6.00 mchana idadi ya wanafunzi waliokutwa na hali hiyo walikuwa zaidi ya 80.
Akithibitisha kuwapokea wagonjwa hao Ofisa Tabibu wa Zahanati ya Kijiji cha Kajana Festo Eliakimu akiri kupokea wanafunzi 70 wakiwa na hali mbaya na kuwapatia huduma ya kwanza lakini alikabiliwa na tatizo la ukosefu wa kipima joto (thermometer) , hali iliyomlazimu aombe kipimo hicho kwa ofisa afya wa Wilaya ya Buhingwe.
“chanzo cha ugonjwa hakijajulikana mapaka leo na wanafunzi 70 nimewapumzisha na kuwapatia huduma ya kwanza, hapa sina vipimo vya joto hivyo nimeomba msaada kwa afisa afya wa Wilaya na amekwisha fika hapa japo baadhi ya wazazi wamewachukua watoto wao na kuwapeleka Hospitali ya shunga ambayo ina vipimo zaidi , baada ya kuona hali zao zinazidi kuwa mbaya” alieleza Eliakimu.
Kwa niaba ya wazazi wa watoto hao Violethi John alisema tukio hilo limewashangaza kwa kuwa ni mara ya kwanza kuona watoto wao wanaumwa wakiwa shule, na kuupongeza uongozi wa shule hiyo, zahanati na Wilaya hiyo kwa ushirikiano walioutoa katika kuokoa maisha ya wanafunzi hao.
No comments