FAIDA ZA MAJI MWILINI
Kuna watu ambao katika maisha yao ya kila siku hawana tabia ya kunywa maji mara kwa mara .Hii ni
kutokana na kuona kero kwa kunywa maji kila wakati au kuona uvivu wa kubeba chupa za maji au kulazimika kufuata mahali ambapo maji yanapatikana lakini kubwa kuliko zote kati ya sababu hizo ni kutofahamu umuhimu wa kunywa maji mara kwa mara katika maisha ya afya ya mwanadamu.Maji ni sehemu muhimu ya maisha ya mwanadamu na yana machango mkubwa sana katika afya ya mwili na kama yakinywewa ipasavyo yanaweza kukuepusha na magonjwa mengi ambayo yatakufanya uishi maisha marefu .Maji yanakufanya uendelee kuonekana mdogo.
Maji yanafanya ngozi yako iwe na vimeleo au mabaki muhimu ya maji muda wote na hivyo kuondoa adha ya ngozi kuharibika kutokana na umri mkubwa . Maji kiasilia hurutubisha ngozi huku ikijazia mistari ambayo huondoa makunyanzi na kuifanya ionekana kuwa nyororo na laini.Unywaji wa maji huondoa Msongo wa mawazo.Unaweza ukashindwa kuamini jinsi gani maji yana mchango kwenye afya ya saikolojia yako lakini ile sauti ya maji yakiwa yanachuruzika inaweza kutuliza mawazo yako na kuondoa msongo wa mawazo .
Maji yasaidia kupunguza na kuponya mafua .Unywaji wa maji husaidia kuondoa mafua kwa wale wenye allergy ya vumbi na uchafu na pia kunawa mikono mara kwa mara kwa maji masafi kunasaidia kuua vijidudu ambavyo huwafanya watu kupata mafua mara kwa mara .Maji yasaidia nywele.Kwa wale wadau wa masuala ya urembo hasa kina dada zaidi ya kuritubisha ngozi maji husaidia kung’arisha nywele . Kuosha nywele kwa maji ambayo hayajachemshwa kwa kutumia virutubisho vya nywele vya kutengeneza kama vile shampoo na mafuta maalum aina ya conditioner yanazifanya nywele kuwa thabiti zaidi na kuondoa uwezekano wa kungoka hovyo hovyo huku zikiwa na mn’gao .Ngozi ya mwili husaidiwa sana na maji.Zaidi ya ngozi ya uso maji ni muhimu kwa ngozi ya mwili kwa ujumla . Wakati wa kuoga maji ya moto au vugu vugu hufanya ngozi ya mwili kuwa nyororo na yenye afya zaidi , maji husaidia kuondoa ukavu ambao huondoa mvuto wa asili wa ngozi na kuipa afya kwa ujumla .Maji husaidia kupunguza uzito wa mwili.Kwa wale wenye matatizo ya uzito ambayo wakati mwingine yanaweza yakawa hatari kwa afya yako kwa kusababisha matatizo kama Presha ,kisukari na magonjwa ya moyo maji yanaweza kuwa kimbilio lako. Kwa kujibu wa utafiti , watu wazima wanaokunywa glasi nane za maji kwa siku yaani angalau glass mbili kwa kila baada ya saa kadhaa hasa kabla ya wakati wa kula wanajikuta wakila chakula kidogo na hivyo kufanya mwili wako kupata chakula kile kile kinachohitajika na mwili wako na hivyo kuondoa uwezekano wa mwili wako kulimbikiza chakula kinachofanya uzito wako uendelee.Maji huisaidia akili kufanya kazi vizuri .Mwili unapokosa maji tatizo pekee sio mtu kuhisi kiu wakati mwingine ubongo huhisi kuchoka kirahisi na haraka pale ambapo mtu hajanywa maji muda mrefu . Hisia kama hasira , uchovu wa akili , kuchanganyikiwa humtokea mtu kirahisi wakati akiwa hajanywa maji muda mrefu na wakati mwingine hata kichwa huuuma sana lakini suluhisho la yote haya ni kunywa maji mara kwa mara .Muwasho wa koo.Muwasho wa koo unaotokana na allergy au mafua hutibiwa na maji , mtu anapopata tatizo hili suluhisho la haraka ni kusukutua maji yenye chumvi lakini kuepsuah tatizo hili ni kuhakikisha koo halikauki kwa muda mrefu .Maji husaidia kupigana dhidi ya magonjwa .Maji yana msaada mkubwa sana kwenye kupambana na magonjwa mwilini mwako . Ni vizuri kunywa maji mara kwa mara kuepusha mwili wako na magonjwa . Pia ulaji wa matunda husaidia kuupa mwili maji muhimu yanayokuwa kinga dhidi ya magonjwa mbalimbali . Matunda kama mapapai,matikiti maji,matango,machungwa ,ndizi,maembe yanauongezea mwili maji ambayo yanakufanya ukae muda mrefu bila kuugua.
No comments