-->

Header Ads

CUF; BODI YA UDHAMINI

Leo October 5, 2016 nimeipata stori hii kutoka Bodi ya udhamini ya chama cha wananchi CUF kuhusu kufungua kesi mahakama kuu dhidi ya msajili wa vyama vya siasa nchini pamoja na Profesa Ibrahim Lipumba kwa madai ya kuingilia mamlaka ya chama hicho.
Taarifa ya Wakili Nassor Juma imesema kuwa bodi ya udhamini ya CUF imefungua shauri hilo ikitaka kupata amri ya mahakama ili kumzuia msajili wa vyama vya siasa nchini, Jaji Francis Mutungi kufanya shughuli za kisiasa nje ya mamlaka aliyopewa na sheria na kanuni za vyama.
Na kwa mujibu wa Wakili huyo amesema shauri hilo limefunguliwa na Bodi ya wadhamini ambao ndiyo wenye maamuzi ya mwisho kuhusu chama.
>>>>Shauri limefunguliwa na bodi ya wadhamini wa chama dhidi ya msajiili wa vyama, Profesa Ibrahim Lipumba na wananchi wengine 12. Bodi ya wadhamini wa chama cha wananchi CUF ni moja tu hivyo msajili hana bodi ya wadhamini tofauti hii ambayo imesajiliwa kwake hivyo walioleta shauri hili mahakamani ni bodi ambao ndiyo wenye mamlaka:- Wakili Nassor

No comments

Powered by Blogger.