Rais mstaafu wa Serikali ya Awamu ya
Nne ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania , Dkt. Jakaya Kikwete amekubali
shamba lake la mifugo lililopo kijijini kwake Msoga Bagamoyo litumike
kama shamba darasa.
Mh.
Jakaya Kikwete amekubali ombi hilo kutoka Chuo Kikuu cha Sokoine cha
Kilimo (SUA) kilichopo mkoani Morogoro, baada ya kutembelea chuoni hapo
akiwa na wataalamu wake wa mifugo kwa lengo la kujifunza mambo
mbalimbali kuhusu kilimo na mifugo.
Uongozi wa SUA ukatumia nfasi hiyo kuwasilisha ombi lao kwa Mh.
Kikwete ambaye alikubali na rasmi kuingia makubaliano ya pamoja ili
kulitumia shamba lake la mifugo kama shamba darasa la kutolea elimu ya
vitendo kwa wanafunzi wao, wataalamu wa mifugo na wafugaji.
Aidha Rais Mstaafu ameeleza kulizishwa na mafunzo aliyoyapata chuoni
hapo na kutoa ahadi ya kuendelea kushirikiana na chuo hicho kwa lengo la
kuleta mabadiliko ya kisayansi ya sekta ya ufugaji iweze kumletea tija
mfugaji.
Rais Mstaafu Kikwete kwa sasa amejikita zaidi kwenye suala la ufugaji
wa kisasa wa ng’ombe wa maziwa, kilimo cha mazao ya chakula na matunda
hasa mananasi kijijini Msoga, Chalinze , wilayani Bagamoyo, mkoa wa
Pwani.
KWA HABARI ZA HIVI PUNDE TANZANIA LEO jiunge na AKISITV na www.akisitv.com updates zote utazikuta humu
No comments