Mtu mmoja anaripotiwa kufariki dunia kutokana na mvua zinazo endelea jijini Dar es Salaam.
Akizungumza
jijini Dar es Salaam Kamanda Mkoa wa kipolisi Ilala Salum Hamduni
ameeleza kuwa mvua zinazo endelea jijini Dar es Salaam zimeweza kupoteza
maisha ya kijana Mmoja maeneo ya Tabata Kimanga, Mto Kenge ambaye
anakadiriwa kuwa na umri kati ya miaka 25 mpaka 30.
RPC
Hamduni ameeleza kuwa taarifa za kijana huyo kuhusu majina yake bado
hazija kamilika, na kuhusu uharibifu wa mali amehaidi kutoa ufafanuzi
hapo baadae.
Mkuu
wa Wilaya ya Ilala Sophia Mjema akimuonesha Mbunge wa jimbo la Ilala
Mussa Hassan Zungu baadhi ya nyumba zilizoharibiwa na mvua (nyumba
hazipo pichani)
Naye
Mkuu wa Wilaya ya Ilala Sophia Mjema amewataka wakazi wote wanaosihi
maeneo hatarishi hususani Jangwani kuondoka mara moja kwani mvua hizi ni
endelevu na huenda zikafika mpaka siku ya Jumamosi hivyo ni vyema
kuchukua tahadhari kwa kuhama maeneo na kwenda maeneo yaliyo salama.
Mtandao
huu ulitembelea eneo la Jangwani na kujionea miundombinu ilivoharibiwa
na kupelekea suala la usafiri kuwa mtihani kwa wakazi wa maeneo mbali
mbali ikiwemo Kimara, Mbezi nakadhalika, huku nyumba nyingi kwa asilimia
kubwa zikiwa zimejaa maji.
Barabara kuelekea Jangwani ikiwa imefungwa
KWA HABARI ZA HIVI PUNDE TANZANIA LEO jiunge na AKISITV na www.akisitv.com updates zote utazikuta humu
No comments