HELIKOPTA YAANGUKA ZIWA NAKURU NCHINI KENYA
Ndege
moja aina ya helikopta imeanguka katika ziwa Nakuru nchini Kenya muda
mfupi baada ya kuondoka katika hoteli moja mjini humo.
Afisa mkuu
wa Polisi mjini Nakuru Joshua Omukata amethibitisha kisa hicho akisema
kuwa walikuwa wakisubiri boti kufanya operesheni ya kuwanusuru waliokuwa
wakiabiri ndege hiyo.Ripoti zinasema kuwa kuliwa na watu watano katika ndege hiyo.
Seneta wa Nakuru Susan Kihika amesema kuwa watatu kati ya wale waliokuwa wameabiri ndege hiyo walikuwa wanachama wa kitengo chake cha mawasiliano.
Ndege hiyo iliondoka katika hoteli ya Jarika County Lodge na duru zinasema kuwa ilikuwa ikipaa chini chini kabla ya kuanguka.
Ndge hiyo ilitarajiwa kusafrisha waandishi wa habari katika mkutano wa kampeni .
Waokoaji walikuwa bado hawajaanza operesheni saa nne baada ya ndege hiyo kuanguka katika ziwa hilo kwa ukosefu wa boti.
Waokojai walilazimika kusubiri boti kusafirishwa kutoka Ziwa Naivasha.
Mkurugenzi wa Idara ya kitaifa ya kukabiliana na majanga Pius Masai amesema kuwa ndege ya polisi imetumwa katika eneo hilo kusaidia katika uokoaji.
KWA HABARI ZA HIVI PUNDE TANZANIA LEO jiunge na AKISITV na www.akisitv.com updates zote utazikuta humu
No comments