Hatimaye bilionea wa IPTL apelekwa Muhimbili
Dar es Salaam. Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa
(Takukuru), imetekeleza amri ya Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu kwa
kumpeleka mshtakiwa wa kesi ya uhujumu uchumi, Harbinder Sethi katika
Hospitali ya Taifa ya Muhimbili (MNH) kufanyiwa vipimo.
Mwendesha
Mashtaka Mwandamizi wa Takukuru, Leonard Swai jana alimweleza Hakimu
Mkazi Mkuu, Huruma Shaidi wakati kesi hiyo ilipokwenda kutajwa.
Alieleza
kuwa wametekeleza amri za mahakama walizopewa kwa kumpeleka Sethi
Muhimbili na kwamba kinachosubiriwa ni ripoti ya daktari.
Naye
wakili wa mshtakiwa James Rugemalira, Respicius Didas alieleza kuwa
kuna ucheleweshaji wa upelelezi na kwamba washtakiwa walifikishwa
mahakamani tangu Juni 19 na wapo ndani hadi sasa.
Wakili
Didas alidai kuwa kila kesi ikifika mahakamani upande wa mashtaka
unawaambia upelelezi bado, wateja wao wanaendelea kukaa ndani na
wameathirika. Akijibu hoja hiyo, Swai alidai uchunguzi wa kesi ya
kughushi unachukua muda na sheria ipo wazi.
Sethi na
Rugemalira wanakabiliwa na mashtaka matano ya kutakatisha fedha pamoja
na kusababisha hasara ya Dola 22,198,544.60 na Sh 309,461,300,158.27.
Hakimu Shaidi aliiahirisha kesi hiyo hadi Oktoba 27 kesi hiyo itakapotajwa.
Share this story
JIUNGE NASI AKISI TV KILA SIKU KUPATA HABARI ZA UHAKIKA Nini maoni yako? Weka comment yako hapa,
No comments