Vibanda 200 vya wavamizi vyateketezwa Kagera
Kamati ya ulinzi na usalama ya wilayani Missenyi mkoani Kagera, imeteketeza kwa moto zaidi ya vibanda 200 ambavyo vilijengwa na wavamizi kwenye mapori ya akiba.
Akiongoza zoezi hilo leo Jumatano Septemba 20, Mkuu wa Wilaya hiyo Kanali Denice Mwilla, amesema mpaka sasa ekari zaidi ya 1000, kati ya 7000, zimevamiwa na watu ambao baadhi yao wanatokea mkoani Kigoma.
Kwa mujibu wa taarifa ya mwandishi wa Azam TV, Junior Mwemezi, aliyepo mkoani Kagera, watu hao wamekiri kukaa eneo hilo kimakosa na kudai kuwa waliuziwa sehemu hizo kwa gharama ya shilingi 300,000.
Wakazi hao wanasema hawakuwa na elimu ya kutosha ya kujua vyema mipaka.
No comments