Baraza la Vijana Chadema (BAVICHA) Watangaza Maandamano

BARAZA la Vijana wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Bavicha) Mkoa wa
Kagera limetangaza kuandaa maandamano ya amani kulaani tukio la
kushambuliwa kwa risasi Mwanasheria Mkuu wa chama chao, Tundu Lissu
Septemba 7, mwaka huu.
Mwenyekiti wa Bavicha Manispaa ya Bukoba, Ishengoma Audax alisema licha
ya kuandamana watakwenda katika Hospitali ya Rufaa Bukoba kuchangia
damu.
Akizungumza kwa niaba ya Mwenyekiti wa Bavicha Mkoa wa Kagera, Francis
Rutta alisema wameamua kuandamana kulaani kushambuliwa kwa Lissu na
kuvitaka vyombo vya dola kuhakikisha vinawakamata na kuwatia mbaroni
wahusika.
“Tunafanya maandamano ya amani hivyo hatutegemei polisi kuzuia maandamano yetu kwa kuwa ni ya amani.
“Lakini tunaunga mkono uamuzi wa Balaza Kuu la Taifa Bavicha linaloongozwa na Mwenyekiti Patrobas Katambi,” alisema.
Alisema wamekuwa wakishangazwa na hatua ya polisi kuwazuia wananchi
kumuombea Tundu Lissu ikiwa ni pamoja na kukamatwa kwa makada wa chama
chao waliovaa fulana zenye ujumbe wa kumuombea.
Alisema huo ni ukiukaji mkubwa wa demokrasia.
JIUNGE NASI AKISI TV KILA SIKU KUPATA HABARI ZA UHAKIKA Nini maoni yako? Weka comment yako hapa,
No comments