RASMI; NIYONZIMA ATUA RASMI AFRIKA KUSINI, AJIUNGA NA KIKOSI CHA SIMBA.
Baada ya sintofahamu na tetesi nyingi juu ya usajil wa Kiungo wa zamani wa Yanga, Horuna Niyonzima sasa atua rasmi Afrika kusini kujiunga na kikosi cha Simba.
Kikosi cha Simba kiliondoka mwanzoni mwa mwa wiki kwa ajili ya kambi ya siku kadhaa kwa ajili ya kujiandaa na msimu mpya wa ligi kuu Tanzania bara.
Habari iliyotufikia AkisiTv kutoka kwa chanzo chetu cha kuaminika ni kuwa Niyonzima tayari ashajiunga na kikosi hicho cha Simba tayari kwa mazoezi ya maandalizi ya msimu ujao.
Niyonzima amejiunga na timu hiyo siku ya jana akitokea kwao Rwanda alipokuwa kwa mapumziko na sasa amejiunga rasmi na timu yetu, kilisema chanzo chetu cha habari.
Bado usajili huo ni unafanywa kwa siri na uongozi wa Simba wamepanga kumtambulisha Niyonzima katika siku ya Simba day itakayofanyika mapema mwezi wa nane.
No comments