IMETHIBITISHWA KUWA CRISTIANO RONALDO ANATARAJIA MTOTO MWENGINE.
Akiongea na kituo cha Hollywood Life kwa niaba ya Cristiano Ronaldo ,muwakilishi wa mwanasoka huyo bwana Ruben Malaret alisema kuwa Cristiano Ronaldo kwa sasa ni mtu mwenye furaha kwani mbali na kupata mapacha wiki kadhaa zilizopita pia anatarajiwa kuitwa baba tena kwani anatarajia kupata mtoto na mpenzi wake. Georgina.
Cristioano Ronaldo ambae kwa sasa anawatoto watatu wakiume anatarajia kupata mtoto wa nne mwezi oktoba mwaka huu, "Cristiano is enjoying every moment with all three of his chidren" alisema Ruben akimaanisha Cristiano anafurahia kila anachofanya na watoto wote watatu alionao.
Ruben alisema Cristiano Ronaldo ambaye wiki kadhaa ziiliopita alibahatika kupata watoto mapacha wa kiume anamsubiri kwa hamu sana mtoto wake mwingine anaaetarajia kumpata na mpenzi wake Georgina huku akithibitsha kuwa kwa sasa Ronaldo ni mtu mwenye furaha sana.
No comments