-->

Header Ads

NINI KINAENDELEA KATI YA KENYA NA IRAN JUU YA UHUSIANO WAO?

Balozi wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran nchini Kenya, Hadi Farajvand amesema kuwa, mahusiano ya Kenya na Iran hususan katika uga wa uchumi, yamestawi sana katika miaka ya hivi karibuni.

Farajvand ameyasema hayo katika dhifa ya futari iliyohudhuriwa na wamiliki wa vyombo vya habari katika ubalozi wa Iran jijini Nairobi ambapo sambamba na kuashiria ongezeko la mashirika ya Iran nchini Kenya amesema kuwa, mahusiano ya nchi mbili katika sekta tofauti yanaendelea kupanuka.


Bandari ya Iran inayosafirisha mizigo kwenda Kenya


Balozi wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran nchini Kenya pia amezungumzia safari ya ujumbe wa benki kuu ya Iran jijini Nairobi itakayofanyika siku kadhaa zijazo kwa ajili ya kufanya mazungumzo na viongozi wa benki kuu ya nchi hiyo mwanachama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki. Balozi wa Iran nchini Kenya ameashiria pia uchaguzi wa rais wa mwezi Agosti mwaka huu nchini humo na kusema kuwa, anatumai kwamba uchaguzi huo utafanyika katika anga ya amani na utulivu.



Hivi karibuni pia, Murtadha Daylan, Mwambata wa kibiashara wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran nchini Kenya akizungumza na Shirika la Habari la IRNA alisema kuwa, Kenya inaongoza katika ununuzi wa bidhaa kutoka Iran barani Afrika na ni ya 15 kwa ujumla katika ununuzi wa bidhaa za Iran duniani.

JIUNGE NASI AKISI TV KILA SIKU KUPATA HABARI ZA UHAKIKA Nini maoni yako? Weka comment yako hapa,

No comments

Powered by Blogger.