-->

Header Ads

MAELFU YA WATOTO KUFARIKI SOMALIA: RIPOTI


Mchini Somalia hali bado so shwari, taasisi moja ya kimataifa ya masuala ya kibinadamu imetoa tahadhari ya kuwepo kwa hatari ya kuaga dunia watoto wa Kisomali elfu 20 kutokana na ukame na njaa iliyoiathiri Somalia.
Mkurugenzi wa taasisi ya Save the Children nchini Somalia  Hassan Noor Saadi amesema kuwa watoto elfu 20 wataaga dunia kwa njaa kali iwapo misaada ya kibinadamu haitapelekwa nchini humo.
Ripoti iliyotolewa na Save the Children imeeleza kuwa, lishe duni inatishia maisha ya nusu ya watoto katika maeneo tisa ya Somalia yaliyokumbwa na ukame.
Mkurugenzi wa taasisi hiyo nchini Somalia ameeleza  kuwa, mvua zilizonyesha hivi karibuni hazikuwa za kutosha na hivyo kuongeza wasiwasi wa kupata chakula kutokana na kukosekana kwa akiba.
Umoja wa Mataifa pia umetangaza kuwa, watu milioni sita na laki saba wanahitaji misaada ya dharura ya kibinadamu huko Somalia na kwamba hali ya mambo inazidi kuwa mbaya zaidi.

No comments

Powered by Blogger.