-->

Header Ads

WANANCHI 100 WAUAWA NA MAMIA WAJERUHIWA SOMALIA

Ripoti kutoka mtandao wa habari wa al Yaum al Saabi' wa nchini Misri zinasema kuwa zaidi ya watu mia moja wameuawa na wengine kujeruhiwa katika mapigano nchini Somalia.

Mtandao huo umemnukuu Muhammad Ali, mkuu wa mkoa wa Jaldadu wa katikati mwa Somalia akisema kuwa, mapigano ya silaha yaliyotokea kwenye mkoa huo yamepelekea watu wasiopungua 6 kuuawa na wengine 99 kujeruhiwa.

Kwa mujibu wa ripoti hiyo, mapigano hayo yametokea kwa lengo la kudhibiti maeneo ya malisho na ya kilimo.

Somalia inahitaji misaada mingi ya dharura kutokana na kukumbwa na majanga mengi yakiwemo ya ukame, mashambulizi ya kundi la kigaidi la al Shabab.

Hatahivyo uchache wa mvua na maradhi, ni kati ya mambo ambayo yamewaongezeka umaskini na njaa wananchi wa nchi hiyo ya Pembe ya Afrika.

No comments

Powered by Blogger.