-->

Header Ads

BREAKING: Kiwanda Chawaka Moto Shinyanga



Kiwanda cha Jambo kilichopo mkoani Shinyanga kimenusurika kuteketea kwa moto baada ya hitilafu ya umeme kutokea kwenye moja ya ghala  lililokuwa na marobota ya pamba.

Kamanda wa jeshi la zima moto na uokoaji mkoani Shinyanga, Omari Simba amesema tukio hilo la moto lilitokea Mei 15 saa tatu 3.00 baada ya hitilafu hiyo kutokea.

Amesema jeshi hilo lilipata taarifa ya tukio hilo kutoka kwa uongozi wa kiwanda hicho kuwa kuna ajali ya moto  ndipo walifika eneo la tukio na kukuta ghala hilo likiungua  huku moto ukianza kusambaa kwa kasi lakini walifanikiwa kuudhibiti kabla ya kusababisha madhara makubwa.

Simba amesema uzimaji wa moto huo ulichukua saa sita huku akitoa rai kwa wananchi na wamiliki wa viwanda kutoa taarifa mapema pindi yanapotokea matukio katika maeneo yao hasa ya moto ili kunusuru kutokea madhara makubwa ambayo yangeweza kuzuiliwa mapema.

Kaimu mkurugenzi wa  kiwanda  cha Jambo, Sulemani Sule hakuwa tayari kuzungumzia tukio hilo baada ya waandishi wa habari kufika kiwandani hapo, na kueleza kuwa  taarifa  watazitoa  watakapomaliza kufanya tathmini ya mali zote zilizoteketea moto.



SHARE THIS STORY

JIUNGE NASI AKISI TV KILA SIKU KUPATA HABARI ZA UHAKIKA Nini maoni yako? Weka comment yako hapa,

No comments

Powered by Blogger.