-->

Header Ads

UCHAFU WAMPONZA, APIGWA FAINI HII


Muleba. 

Hatua ya Serikali kudhibiti uchafu, imesababisha wakazi watano wa Kijiji cha Kamachumu, Wilaya ya Muleba mkoani Kagera, wametozwa faini ya Sh250,000.

Adhabu hiyo imetolewa baada ya Kamati ya Afya na Usafi wa Mazingira kufanya ukaguzi katika mji wa Kamachumu.
Faini hiyo ilitozwa baada ya kamati hiyo ya wilaya kufanya ukaguzi kwa mara ya pili.
Ofisa Afya Wilaya ya Muleba, Projestus Rugaimukamu alisema wananchi hao walikutwa bila mashimo ya kutupa taka, vyoo na mitaro ya kupitisha maji machafu ikiwa imeziba.

Mkuu wa Wilaya ya Muleba, Richard Ruyango aliwataka viongozi wa vijiji na maofisa afya na usafi wa mazingira kufuatilia maagizo yanayotolewa ma mamlaka za Serikali ya kutunza na kuhifadhi mazingira, anayekaidi akamatwe na kuchukuliwa hatua za kisheria


CREDIT; MWANANCHI

JIUNGE NASI AKISI TV KILA SIKU KUPATA HABARI ZA UHAKIKA Nini maoni yako? Weka comment yako hapa,
Powered by Blogger.