-->

Header Ads

MBINU ZA JESHI LA SYRIA MPAKA KUUWA MAGAIDI



Jeshi la Syria huku likiungwa mkono na vikosi vya anga vya nchi hiyo limewauwa makumi ya magaidi katika oparesheni ya kuukomboa mji wa Halfaya na kuwasababishia hasara kubwa magaidi hao.

Jeshi la Syria na brigedi za muqawama wa Kiislamu jana Jumatatu zilianzisha oparesheni ya kuukomboa mji wa Halfaya kaskazini mwa mji wa Hama kwa lengo la kuwafurusha wanamgambo wenye silaha huku vikosi vya Syria vikiendelea kusonga mbele katika eneo hilo. 

Katika upande mwingine, imeelezwa kuwa ndege za kivita za Syria zilishambulia kambi na ngome za magaidi wakufurishaji kwa zaidi ya mara 16 katika maeneo ya Juber, Ain Tarma na Qaabun huko Damascus.

Wakati huo huo vikosi vya jeshi la Syria vimeanza oparesheni ya kulikomboa eneo la kiistratejia la kambi ya kijeshi la  Abu Dhuhur na katika bwawa la Abu Qala la mashariki mwa Homs, magharibi mwa Syria. 

No comments

Powered by Blogger.