JINSI YA KUPIKA CHAKULA KIZURI CHA PILAU YA MAYAI
LEO kwenye kona hii nimekuletea jinsi ya kupika pilau ya mayai ya kuchemsha kwa kuyachanganya na viazi. Hapa mayai yanaingia badala ya viazi.
MAHITAJI
Chukua mchele kilo moja, mayai matano, viungo vya pilau vilivyosagwa, mafuta ya kupikia, viungo ambavyo havijasagwa vya pilau, pia maji yaliyochemshwa. Zabibu kavu, vitunguu swaumu na vitunguu maji vilivyokatwa vipande vikubwavikubwa.
MAANDALIZI
Pilau ya mayai na zabibu kavu mayai yako kisha yakaange mpaka yawe na rangi ya kahawia au ‘braun’.
WAKATI WA KUPIKA
Sasa chukua mafuta, yaweke kwenye jiko, yachemke, baada ya kuchemka weka vitunguu maji, vikaange mpaka viwe brauni. Baada ya hapo weka kitunguu swaumu, kikaange mpaka kiishie, ukimaliza weka viungo vilivyosagwa, kaanga hadi viive vizuri kisha weka mchele, ukaange mpaka uingie viungo vyote.
Ukimaliza, weka viungo vizima, vikaange kidogo kisha weka maji. Pilau likishakaukia maji kama limeanza kuiva weka mayai kama unayatumbukiza ili ukiwa katika hatua ya kupalia mkaa au kuweka kwenye oven, mayai nayo yachanganyike na pilau lako.
Kumbuka mayai hayatakiwi kuwekwa wakati kukiwa bado kuna maji. Acha kwa muda wa nusu saa kisha toa, geuza pilau lako ambalo sasa litakuwa tayari kwa kuliwa. Wakati wa kugeuza ndio unatupia zabibu kavu zinazoleta utamu kwenye pilau.
No comments