-->

Header Ads

BREAKING : MAJAMBAZI WAUWA ASKARI POLISI WATATU MKURANGA




Habari zilizotufikia hivi punde, zimeeleza kuwa, askari polisi watatu wameuawa na majambazi huko Mkuranga, Mkoani Pwani.

Habari hizo zinasema kuwa, askari hao wameuawa kwa kupigwa risasi na majambazi hao wakati wakijiandaa kuondoka kwenye lindo ambalo lilikuwa ni kizuizi cha barabarani ili warudi kituoni. 

Imeelezwa kwamba majambazi hao waliwavamia ghafla polisi hao waliokuwa kwenye gari na kuwapiga risasi na kuwaua wote palepale eneo la tukio, kisha kutokomea kusikojulikana.

HATAHIVYO BADO HAKUNA TAARIFA RASMI KUTOKA JESHI LA POLISI..

No comments

Powered by Blogger.