-->

Header Ads

BINADAMU KUISHI KATIKA SAYARI YA SATURN?? WANASAYANSI WAGUNDUA HILI.

Mdau wa AKISITV nimeona leo nkufahamishe juu ya kuwepo kwa sayari ambayo imeonekana kuwa na uwezo wa kuishi viumbe hai.
Katika sayari hii mwezi wa Enceladus ambao uko kwenye sayari ya Saturn unasemwa huenda ukawa mahali bora zaidi pa kwenda kutafuta maisha nje ya dunia.


Tathmini hii imetolewa kufuatia uchunguzi katika sayari hiyo yenye kilomita 500 uliofanywa na Cassini.
Hatahivyo uchambuzi wa kemia wa Cassini unaonyesha matundu ya maji moto kwenye sakafu ya bahari ya Enceladus, maeneo ambayo yanahusishwa na kuwepo kwa maisha, hapa duniani.
Kuwepo kwa maji haya sio thibitisho kamili kwamba vitu vilivyo na uhai vinaishi katika mwezi huo mdogo lakini teknolojia zinaweza kutumika kupima maji hayo na kutoa ushahidi zaidi.
Bahari iliyopo kwenye Enceladus inakisiwa kuwa na kina kirefusana sana na yapo majimaji kwa sababu ya joto linalotokana na mvuto wa mara kwa mara kutoka kwenye sayari ya Saturn.
Cassini tayari amedhibitisha kwamba maji hayo yanashikana na sakafu ya bahari kutokana na aina ya chumvi na silika ambayo pia imeonekana katika mashimo.
Lakini wanachotaka kujua sana wanasayansi ni ikiwa maswala fulani yanayotendeka duniani pia yanaweza kufanyika katika Enceladus - kitu kinachoitwa serpentinisation, ambayo hutengeneza gesi ya hidrojeni.
Viumbe hai anavyozungumzia Dkt McKay vinaitwa methanojeni kwa sababu vinatengeneza gesi ya metheni vinapogusana na hidrojeni na gesi ya kaboni .
Nasa, ambayo inaongoza ujumbe wa Cassini , ilitakikana kufanya tangazo la hidrojeni miezi michache baada ya uchunguzi wa mwisho waroketi ya mwezini, Oktoba mwaka wa 2015.

Ziara ya Cassini sasa inakamilika . Baada ya kuizunguka Saturn kwa muda wa miaka 12, inaendelea kuishiwa na mafuta na sasa itawachiliwa kuingia kwenye anga ya dunia hiyo ya Saturn mwezi Septemba, kuhakikisha kuwa haiwezi kugongana na Enceladus na kusababisha kuchafuka kwake.

No comments

Powered by Blogger.