Tetesi na habari za uhamisho na usajili kutoka Ligi Kuu Uingereza, La Liga, Serie A, Bundesliga na kwingineko.
Niaje mdau wangu wa kona hii ya michezo, leo nimekuletea muhtasari wa tetesi na habari za uhamisho na usajili kutoka Ligi Kuu Uingereza, La Liga, Serie A, Bundesliga na kwingineko.. Twende wote tuone..kisha mwisho weka comment yako hapo chini...
CHELSEA YAMFUKUZIA ALEXIS
Alexis Sanchez Arsenal Premier League
Meneja wa Chelsea Antonio Conte amelenga kumsajili mchezaji wa Arsenal Alexis Sanchez majira ya joto kwa mujibu wa habari kutoka The Guardian.
Muitaliano huyo kwa sasa anafanya mazungumzo ya mkataba mpya na klabu yake na ameshafanya mjadala kuhusu maswala ya uhamisho na uongozi wa klabu ya Chelsea, hivyo kuwa mstari wa mbele kumpata mchezaji huyo raia wa Chile anayetaka kuondoka Emirates majira ya joto.
Alexis amekerwa na kikosi cha Arsenal kisicho na maendeleo, pia anatakiwa na PSG, Juventus na Inter Milan.
HAZARD ANAJIFUNZA KIHISPANIOLA KABLA YA KUTUA MADRID
Eden Hazard, Chelsea
Eden Hazard anajifunza lugha ya Kihispaniola Real Madrid inapoendelea kuifukuzia saini yake kwa mujibu wa Metro.
Hazard, 26, ametengewa kitita cha paundi milioni 100 na miamba hao wa La Liga, na angependa kufanya kazi na Zinedine Zidane.
Chelsea kwa upande mwingine wanatamani kumtia kitanzi cha mkataba mpya, lakini inaaminika Mbelgiji huyo tayari anajiandaa k
BAYERN KUTOA DAU KWA AJILI YA ALEXIS
Alexis Sanchez Arsenal Premier League
Bayern Munich wanataka kumsajili mshambulizi wa Arsenal Alexis Sanchez ingawa watakabiliwa na ushindi kutoka kwa Barcelona na Real Madrid kwa mujibu wa Daily Star.
Mchezaji huyo wa kimataifa wa Chile anamaliza muda wake 2018, na baada ya mazungumzo ya kuongeza mkataba Arsenal kutofikia muafaka, Carlo Ancelotti anaona ndio fursa sahihi ya kumpata nyota huyo.
ARSENAL YAMTENGEA DAU PATRICIO
UEFA Team of the Year Rui Patricio
Arsenal inaandaa kitita cha €15 millioni (£13m) kwa ajili ya kipa wa Ureno na Sporting Rui Patricio, kwa mujibu wa RMC Sport.
Patricio mwenye umri wa miaka 29 tu alishinda Euro 2016 akiwa na nchi yake msimu uliopita wa majira ya joto, pia Marseille wanaiwania saini yake.
BARCA WAMTAKA LEMAR
HD Thomas Lemar Monaco
Barcelona na Atletico Madrid zinamfukuzia winga wa Monaco Thomas Lemar, L'Equipe limeripoti.
Chelsea na Liverpool ndizo timu za Uingereza zinazovutiwa na mchezaji huyo, lakini inaaminika kwamba Mfaransa huyo angependa zaidi kucheza La Liga, ambako Atleti walishatoa kitita cha euro milioni 25 msimu uliopita.
SIGURDSSON KUTIMKIA NEWCASTLE?
Gylfi Sigurdsson Swansea City Premier League
Newcastle wakiwa wanarejea Ligi Kuu Uingereza, watakuwa wakitafuta fursa ya kuipata saini ya Gylfi Sigurdsson kutoka Swansea kwa mujibu wa The Star.
Rafa Benitez yupo tayari kutumia kitita cha paundi milioni 15 kumpata mchezaji huyu, ambaye meneja wake Paul Clement amesema anastahili kujiunga na moja ya klabu kubwa zaidi za Ulaya.
UNITED KUTUMIA €200M KUMSAJILI NEYMAR
Neymar, Barcelona
Manchester United imejiandaa kumlipia Neymar kiasi cha €200 millioni ambayo Barcelona wanaitaka kumwachilia Mbrazili huyo, chanzo cha Hispania Sport kimeripoti.
Sanjari na kuifunika rekodi ya Paul Pogba, Mashetani Wekundu wapo tayari kumfanya Neymar kuwa mchezaji anayelipwa zaidi katika Ligi Kuu Uingereza kwa dili la paundi 415,000 kwa wiki.
BAKAYOKO NA CHELSEA KIMEELEWEKA
Tiemoue Bakayoko
Chelsea wamefikia makubaliano kumsajili kiungo wa kati wa Monaco Tiemoue Bakayoko, kwa mujibu wa TuttoMercatoWeb.
Blues wanaaminika kutoa kitita cha euro milioni 40 kumsajili nyota huyo mwenye miaka 22 taarifa chache zikiwa zinasubiriwa kabla ya dili kukamilika.
BAYERN WANATAKA €90M KUMUUZA THIAGO
Thiago
Barcelona wameambiwa kwamba ni lazima walipe zaidi ya euro milioni 90 ili kuweza kuipata saini ya Thiago Alcantara kutoka Bayern Munich.
Blaugrana wapo sokoni kutafuta mrithi wa Xavi na Andres Iniesta lakini hawawezi kufikia thamani ya fedha inayotakiwa na mabingwa wa Bundesliga kwa mchezaji wao wa zamani.
WILSHERE KWENDA MILAN KUPITIA BECKHAM?
Jack Wilshere Bournemouth
Jack Wilshere anatamani kutimkia AC Milan baada ya klabu hiyo kupendekezwa na nyota wa zamani wa kimataifa wa Uingereza David Beckham, Daily Mail limeripoti.
Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 25 bado amebakiwa na mwaka mmoja kwenye mkataba wake wa paundi 90,000 kwa wiki Arsenal lakini hawezi kufanya uchaguzi hadi Arsene Wenger atakapofanya maamuzi juu ya mustakabali wake.
REAL MADRID YAANZA MAZUNGUMZO NA HAZARD
Chelsea West Ham Eden Hazard
Real Madrid imeanza mazungumzo na nyota wa Chelsea Eden Hazard, kwa mujibu wa Marca, na yanaonekana kuwa na maendeleo mazuri.
Zinedine Zidane anashauku ya kumsajili Mbelgiji huyo aliyempendekeza mwaka 2012, ingawa upatikanaji wake utategemeana na mapenzi ya Antonio Conte iwapo atamhitaji James Rodriguez.
ARSENAL INAMTAKA SCHMEICHEL
HD Kasper Schmeichel Leicester City
Arsenal inataka kumsajili mlinda mlango wa Leicester City Kasper Schmeichel usajili wa majira ya joto kwa mujibu wa the Mirror.
Mchezaji huyo wa kimataifa wa Denmark amekuwa mhimili mkubwa kwa Leicester kushinda taji la Ligi Kuu Uingereza na kutinga hatua ya robo fainali Ligi ya Mabingwa Ulaya hali kadhalika.
Arsene Wenger na wakuu wa Arsenal wapo katika mchakato wa kutafuta mrithi wa kudumu wa Petr Cech, ambaye anakaribia kutimiza miaka 35.
THAMANI YA MBAPPE NI PAUNDI 130M
Kylian Mbappe Monaco
Monaco imetaja thamani ya kiasi wanachotaka kutoka kwa klabu yoyote itakayohitaji kumsajili Kylian Mbappe, kwa mujibu wa Express, klabu hiyo ya Ligiue 1 imetaja dau lake kuwa paundi milioni 130..
Klabu kadhaa katika Uingereza, Ufaransa na Hispania zinatamani kuipata huduma ya nyota huyo wa miaka 18, lakini Manchester United inadaiwa kuongoza mbio za kumfukuzia nyota huyo.
CITY KUTOA PAUNDI MILIONI 50 KUMSAJILI ROSE
Danny Rose, Tottenham
Bosi wa Man City Pep Guardiola anaamini atafanikiwa kumsajili beki wa kushoto wa Tottenham Danny Rose kwa kitita cha paundi milioni 50 dirisha la uhamisho majira ya joto kwa mujibu wa gazeti la Mirror.
Ikiwa dili hilo litafanikiwa, Tottenham watamwendea Luke Shaw kama mbadala wake, kwani Shaw kwa namna yoyote ataondoka Manchester Unted mwisho wa msimu.
MESSI AMZUIA ALBA KUONDOKA BARCA
HD Jordi Alba
Chanzo cha Hispania Diario Gol kimedai kuwa Lionel Messi anafanya jitihada kuizua Barcelona kumuuza Jordi Alba kwa Manchester United.
Ripoti hizo zinadai kuwa Messi hafurahii hali waliyo nayo sasa baada ya kushindwa kuziba pengo la Dani Alves upande wa kulia na hawatakiwi kurudia kosa hilo kuwapa silaha wapinzani wao.
NAVAS KUREJEA SEVILLA
HD Jesus Navas Manchester City
Jesus Navas wa Man City anajiandaa kurejea Sevilla majira ya joto kwa mujibu wa habari kutoka chanzo cha Hispania AS.
Baada ya miaka minne katika Ligi ya Uingereza na kukosa nafasi kikosi cha kwanza Manchester City, Navas mwenye umri wa miaka 31 anaona sasa ni wakati sahihi kurejea La Liga.
JAMES RODRIGUEZ KUTIMKIA LIVERPOOL
James Rodriguez Eibar Real Madrid LaLiga 04032017Nyota wa Real Madrid James Rodriguez ameibukia kuwa mchezaji nambari moja anayewindwa na Liverpool ikiwa watafanikiwa kutinga kwenye michuano ya Ligi ya Mabingwa Ulaya msimu ujao kwa mujibu wa habari kutoka the Mirror.
Nyota huyo wa kimataifa wa Colombia anaangalia mahali pa kwenda ili aachane na miamba hao wa Madrid kwani Zidane haonekani kushawishiwa na kiwango chake.
Rodriguez ameanza mechi saba tu La Liga msimu huu chini ya kiungo huyo wa zamani wa Ufaransa.
MARSEILLE YAMFUKUZIA CASILLAS
IKER CASILLAS | Porto
Marseille inataka kumsajili kipa wa zamani wa Real Madrid Iker Casillas mwisho wa msimu huu kwa mujibu wa A Bola.
Katika umri wa miaka 35 amekuwa katika kiwango bora katika kikosi cha Porto, akiwawezesha kufika hatua ya mtoano Ligi ya Mabingwa, lakini Marseille wanataka kumshawishi kutua Ufaransa kwa ofa ya mkataba wa miaka miwili.
BARCA YAANZA MAZUNGUMZO NA COUTINHO
HD Phil Coutinho
Barcelona wamepiga hatua katika harakati zao kumsajili kiungo wa Liverpool Philippe Coutinho kwa kuanza mazungumzo na wakala wa Mbrazili huyo kwa mujibu wa Sport.
Miamba hao wa La Liga wamekuwa wakimfuatilia nyota huyo wa Liverpool kwa muda mrefu na wanaamini watampata mchezaji huyo licha ya masharti magumu ya Liverpool.
HAZARD KUPEWA DILI JIPYA CHELSEA
Eden Hazard Chelsea 06032017
Chelsea wanamwandalia mkataba mpya Eden Hazard ikiwa ni harakati za kuzizuia timu zinazotaka kumnunua Real Madrid miongoni mwao, limeripoti Daily Mirror.
Blues wanaamini Mbelgiji huyo atabaki, lakini wamejipanga kumtunuku ofa nono kutokana na kiwango chake safi.

No comments