-->

Header Ads

Polisi: "Tunaendelea kukamata wanaomuombea Lissu"

Kamanda wa Polisi Kanda maalum Lazaro Mambosasa, amesema jeshi la polisi linaendelea kukamata watu wanaofanya maombi kwa ajili ya Tundu Lissu.

Kamanda Mambosasa ametoa kaui hiyo leo alipokuwa akizungumza na mwandishi wa East Africa Television, na kusema kwamba 'operation' ya kuwakamata watu hao inaendelea, na jeshi la polisi litatoa idadi rasmi watakapomaliza jukumu hilo.

"Bado tunaendelea kuwakamata, operation inaendelea na tutatoa ripoti mara baada ya kumaliza tukio", amesema Kamanda Mambosasa.

Leo asubuhi jeshi la Polisi limewakamata baadhi ya raia katika eneo la viwanja vya TIP Sinza jijini Dar es salaam, kwa tuhuma za kufanya mikutano isiyo rasmi kumuombea Mbunge wa Singida Mashariki Tundu Lissu ambaye amepigwa na risasi, kitendo ambacho walikipiga marufuku.

No comments

Powered by Blogger.