-->

Header Ads

TIMU ZAFUNGIWA KUTOSHIRIKI UEFA MIAKA MIWILI.


Shirikisho la soka Barani Ulaya UEFA leo limetangaza kuzifungia klabu za Lyon na Besiktas kushiriki michuano ya Ulaya kwa miaka miwili kufuatia mashabiki wao kugombana uwanjani katika mechi yao ya robo fainali Europa Ligi iliyopigwa huko France April,13
na kusababisha mchezo huo kuchelewa kuanza kwa dakika 45.

Pia kila klabu imepigwa faini ya Euro 100,000 (Pauni 83,800). Lyon walishinda mechi hiyo kwa goli 2-1, na mechi ya marudiano itapigwa kesho nchini Uturuki nyumbani kwa Beskitas.

No comments

Powered by Blogger.