-->

Header Ads

EDEN HAZARD AKUBALI KUTUA REAL MADRID

Taarifa kutoka nchini Uingereza zinasema hatimaye Eden Hazard baada ya kukaa kimya kwa muda,sasa amekubali dili la kujiunga na Real Madrid kwa uhamisho ambao unaweza kuweka rekodi ya dunia.

Taarifa zinadai Hazard ameshaanza hadi kutafuta mahala pa kuishi katika mitaa ya Madrid na anasubiri tu msimu uishe ili aende zake kumalizana na Real Madrid.

Zinedine Zidane kwa misimu kadhaa sasa tangu hajawa kocha mkuu alishasema waziwazi juu ya mapenzi yake kwa Hazard na inasemekana Zidane amefanya kazi kubwa kumshawishi Hazard.
Hazard ambaye msimu huu amekuwa nguzo muhimu sana kwa Chelsea na kuifanya kuongoza ligi hadi sasa, anatarajia kusaini Madrid kwa dau la £ 100m ambayo itavunja ile rekodi ya uhamisho aliyonayo Pogba kwa sasa.

Lakini Real Madrid hawamchukui hivihivi Hazard kwani nao watawauzia Chelsea James Rodriguez kama sehemu ya uhamisho huo, ambapo Chelsea nao watato hela ndefu kumchukua Rodriguez.
Sio tu Rodriguez anayetakiwa Chelsea bali pia Alvaro Morata atatumika katika dili hilo kama sehemu ya mabadilishano kati ya vilabu hivyo viwili, Hazard sasa anaenda kuwa mmoja kati ya nyota watakaokuwa wapewa pesa nyingi Madrid kama ilivyo kwa Bale na Ronaldo

No comments

Powered by Blogger.